Tuesday 27 February 2018

Wasaidizi wa Ikulu ya Marekani wamlalamikia binti wa Rais Trump



Ikulu ya Marekani inanukia mgogoro mkubwa wa kiongozi baada ya wasaidizi wengi wa Rais Donald Trump kulalamika kuingiliwa kazi zao na binti yake, Ivanka.
Mbali na Ivanka, wasaidizi hao wanamlaumu mumewe, Jared Kushner kwa kuongeza dalili za kuwepo mgogoro huo.
Ivanka na Jared waliteuliwa na Trump kuwa washauri wake wakuu ambao hawalipwi mishahara.
Taarifa hizo zimeibuka baada ya CNN kuandika habari yake ya uchunguzi kuhusu utendaji wa binti na mkwe wa Trump, ambao wamekuwa wakilalamikiwa kuingilia majukumu ya wasaidizi wa Rais Trump.
Hata hivyo, Ikulu ya Marekani imekuwa ikikanusha Ivanka na Jared kuingilia kazi za wasaidizi wa Rais Trump.

0 comments:

Post a Comment