Friday 16 March 2018

Amber rose,21 Savage waachana rasmi



Mwanamitindo kutoka nchini Marekani Amber Rose kupitia ukurasa wake wa Instagram ametangaza rasmi kuachana na mpenzi wake 21 Savage.

Amber rose amebainisha sababu za yeye kuachana na 21 Savage ikiwa pamoja na kutaka kuwa huru ili kufanya biashara zake bila kubughudhiwa na mahusiano yoyote.

"Nilitamani tukae muda mrefu katika mahusiano yetu sema kwa sasa nataka kujihusisha biashara zangu bila kuwa na mahusiano," aliandika Amber Rose.
Wawili hao walionekana Mara ya mwisho wakiwa pamoja katika Siku ya wapendanao jimbo la Calfornia.
.

0 comments:

Post a Comment