Thursday 29 March 2018

Angelina Jolie katika mahusiano mapya


Staa wa filamu kutoka nchini Marekani Angelina Jolie ameingia katika uhusiano mpya tangu kuachana na mpenzi wake wa zamani,Brad Pitt mwanzoni mwaka Jana.

Siku za karibuni mrembo huyo alionekana na mwanaume ambaye anadaiwa kuwa ni mpenzi wake mpya anayejushughulisha na udalali wa majumba ya kifahari Jimbo la Texas.

Swahiba wa karibu wa Jolie alivyoulizwa na mtandao wa ET Online alikiri kuwa ni kweli rafiki yake yupo katika mahusiano mapya.

0 comments:

Post a Comment