Thursday 29 March 2018

Paul Okoye asitisha kutoa albamu akiogopa mashabiki



Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria, Paul Okoye ambaye kwasasa anatumia jina la Rude boy baada ya kundi la P square kufa,amesitisha mpango wake wa kuachia albamu yake mwaka huu.

Rude Boy akizungumza na mtandao wa Instablog nija amesema kuwa alikuwa na lengo la kuachia albamu mwaka huu lakini amesitisha kwa kuogopa mashabiki kusema kuwa iliandaliwa tangu kundi la P square likiwa hai jambo ambalo lingemfanya kuonekana kama ndie aliyesababisha kufa kwa kundi.

"Ninasitisha kuachia albamu yangu mpya mwaka huu kwani mashabiki wanaweza kusema nimetengeneza nyimbo hizo toka mwaka 2017 nikiwa katika kundi la P square," amesema Paul.

0 comments:

Post a Comment