Monday 19 March 2018

Diamond kukubali kufungwa jela kwaajili ya Bongo Fleva



Msanii wa Bongo Fleva nchini Diamond Platnumz kupitia kipindi cha radio cha #Theplaylist ya #timesfm amtupia lawama naibu waziri wa habari, sanaa tamaduni na michezo, Mhe Juliana Shonza kuwa anafanya kazi kwa kukurupuka.
.
. "Siogopi kwenda jela kwa sababu ya bongo flava, kwa sababu bongo flava ndiyo baba yangu na ndiyo mama yangu sasa mtu analala akiamka anakuja kufungia kazi zangu wakati serikali imepanga muda halisi wa kurusha katika TV na radio, hata Kama kiongozi kanizidi elimu na wadhifa lakini elimu ya sanaa mimi nimemzidi, awe mpole aite watu Kama Alikiba, fid q, Weusi au Vanessa mdee ili wampe elimu ya sanaa na sio kuchukua maamuzi ya haraka"alisema Diamond
.
.
Pia diamond Platnumz aliongeza kuwa yeye na Wema Sepetu ni wana kwa sasa hawapo kwenye mahusiano.
.
"Nafurahi kuona wakinipa support kina Jokate,Wema na Rose Ndauka mimi siwezi kuwa kwenye mahusiano kwa sababu yalishanishinda"

0 comments:

Post a Comment