Shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) limetangaza kikosi bora cha
wiki hii kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya ambapo klabu mbili
kutoka Uingereza za Chelsea na Manchester United zimefanikiwa kutoa
mchezaji mmoja mmoja huku Bayern wakiambulia patupu. Kwenye kikosi hicho
Klabu ya Barcelona ndio klabu iliyotoa wachezaji wengi (4) ikifuatiwa
na Roma wachezaji watatu na Bestikas mchezaji mmoja. Kwenye kikosi hicho
ambacho wanaangalia mchango wa mchezaji mmoja mmoja kwenye nafasi yake
klabu ya Bayern haijafanikiwa kuingiza mchezaji hata mmoja ingawaje juzi
Machi 14, 2018 wameichabanga Beskitas magoli 3-1 .
0 comments:
Post a Comment