Tuesday 13 March 2018

Michael Carrick kustaafu soka msimu huu



Kiungo wa Manchester United Michael Carrick amethibitisha kustaafu kucheza soka mwisho wa msimu huu 2017/2018

Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza ametangaza hivyo leo wakati wa mkutano wa waandishi wa habari na Klabu yake ya Manchester Utd kuelekea mchezo wa marudiano na Klabu ya Sevilla katika michuano ya UEFA
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 atajiunga na benchi la ufundi la Klabu hiyo ya Manchester Utd baada ya kustaafu

Carrick alianza maisha yake ya soka katika klabu ya Wallsend Boys Club(1986-1997) kisha kuenda Klabu ya West Ham Utd(1997-2004). Baada ya hapo alijiunga na Tottenham Hotspurs(2004-2006) kisha 2006 kujiunga na Manchester Utd


Katika maisha yake ya soka kwenye ligi kuu nchini England, Carrick mpaka sasa amecheza michezo 480, amefunga magoli 24, amepiga pasi za mwisho zilizozaa magoli 40 na kushinda mataji matano

0 comments:

Post a Comment