Wednesday 7 March 2018

Mkataba wa Neymar na Nike wavuja


Wakati Neymar anayeichezea Paris Saint Germain akiwa majeruhi, mkataba wake na kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike umevuja, mkataba wa Neymar na Nike unaonesha kila kitu atakachopewa katika soka kuanzia sasa. Mwanzo Nike walikuwa wakimlipa kiasi cha €40m kwa mwaka na sasa Nike wako tayari kumpatia Neymar $1million kama atachukua tuzo ya mchezaji bora wa dunia (Ballon D'or) mwakani kama Bonus. Kiasi hiki ambacho Neymar atapewa na Nike kama akichukua Ballon D'Or kitakuwa kikiongezeka kwa 100% kila mwaka atakayobeba tuzo hiyo na hii ina maana kwamba hadi 2022 anaweza pokea hadi bonus $4million. Nike hawajaishia hapo kwani bado wana mpunga mrefu wameutenga kwa ajili ya mchezaji huyo wa Kibrazil katika michuano ya kombe la dunia inayotarajiwa kuanza hivi karibuni nchini Urusi. Endapo Neymar atabeba kombe la dunia Nike watamkabidhi kiasi cha $50,000 na kama nyota huyo atamaliza michuano hiyo mikubwa zaidi duniani akiwa kama mfungaji bora wa michuano hiyo atachukua $200,000.

0 comments:

Post a Comment