Wednesday 7 March 2018

Iraq,NATO kuendelea na ushirikiano katika mapambano dhidi ya kundi la IS


Waziri mkuu wa Iraq Bw. Haider al-Abadi jana alikutana na kufanya mazungumzo na katibu mkuu wa jumuiya ya NATO Bw. Jens Stoltenberg ambaye yuko ziarani nchini Iraq, na wamekubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano katika mapambano dhidi ya kundi la IS.
Bw. Abadi amesema, Iraq inahitaji kuendelea kulinda mafanikio yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya kundi la IS, kuondoa itikadi ya ugaidi, na kuwakamata watu wenye msimamo mkali.
Kwa upande wake, Bw. Stoltenberg amesema NATO itaendelea kuiunga mkono Iraq na kufanya ushirikiano katika mafunzo ya askari na ujenzi wa vyuo vya kijeshi.

0 comments:

Post a Comment