Monday 5 March 2018

Mtatiro atimuliwa CUF



Kada wa Chama cha Wananchi(CUF) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya uongozi ya chama hicho, Julius Mtatiro amevuliwa uanachama wa chama hicho jana Machi 4, 2018

Chama kimefikia uamuzi huo kutokana na Mtatiro kukaidi agizo la chama lililomtaka kujibu tuhuma mbalimbali zinazomkabili, mbele ya baraza la utendaji la wilaya ya Ubungo
Mnamo tarehe 20 Desemba 2017, Kamati ya utendaji ya chama hicho iliketi ambapo ilimtaka Mtatiro, na wenzake 6 kuenda mbele ya Kamati hiyo kujibu tuhuma mbalimbali zinazowakabili, agizo ambalo Mtatiro na wenzake walikaidi

Moja ya kosa lililosababisha Mtatiro kuitwa mbele ya Kamati ni kutolipia kadi yake ya uanachama kwa muda wa miaka mitatu sasa, kitendo ambacho ni kinyume na katiba ya chama hicho

Kosa lingine ni kukihujumu (kukisaliti) chama kwa kushirikiana na chama cha CHADEMA katika chaguzi za marudio zilizofanyika ndani ya wilaya ya Ubungo, ambapo licha ya chama hicho kusimamisha wagombea, Mtatiro na wenzake hawakuwaunga mkono

0 comments:

Post a Comment