Michezo ya marudiano ya michuano
ya ligi ya mabingwa Ulaya ilichezwa usiku wa March 6 barani Ulaya kwa
michezo miwili kupigwa, Paris Saint Germain ya Ufaransa wao walikuwa
wenyeji wa Real Madrid ya Hispania wakati Liverpool walikuwa wenyeji wa
FC Porto ya Ureno katika uwanja wa Anfield.
Mchezo kati ya PSG dhidi ya Real Madrid, Madrid wakiongozwa na staa
wao Cristiano Ronaldo wamefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali kwa
kupata ushindi wa magoli 2-1, magoli ya Real Madrid yakifungwa na
Cristiano Ronaldo dakika ya 51, Casemiro dakika ya 80 wakati goli la PSG
lilifungwa na Edinson Cavani dakika ya 71.
Nazo Liverpool na FC Porto zimetoka sare ya bila kufungana.
0 comments:
Post a Comment