Wednesday 7 March 2018

Gonjwa la hatari laibuka Afrika Kusini


 Watu wapatao 1000 wameambukizwa ugonjwa wa Listeriosis  na 180 miongoni mwao wamefariki
Kufuatia tahadhari ya Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa(WHO) juu ya kuenea kwa ugonjwa wa Listeriosis, ambao imebainika kuwa chanzo chake ni nyama inayosindikwa na kiwanda kilichoko nchini humo kiitwacho Food Enterprise

Nchi nne za Kusini mwa Afrika zimesimamisha uagizaji wa nyama ya kuku iliyogandishwa kutoka Afrika Kusini. Nchi hizo ni pamoja na Msumbiji na Zambia

Wauzaji wa maduka wameziondoa bidhaa zinazotoka katika kiwanda cha Food Enterprise kilicho umbali wa kilometa 300 Kaskazini mwa mji wa Pretoria nchini humo

Waziri wa afya wa Afrika Kusini Aaron Motsoa-ledi amewashauri watu kuepuka nyama yoyote ambayo inauzwa ikiwa tayari kuliwa

Listeriosis huathiri wanyama mbalimbali. Maambukizi ya Listeriosis kwa wanadamu hutokea kupitia matumizi ya vyakula vilivyoathirika, hasa maziwa ambayo hayajatibiwa(unpasteurized milk), jibini laini na bidhaa za nyama za kusindika

0 comments:

Post a Comment