Friday 30 March 2018

Roma aimalizia salama kwaresma,Waziri Mwakyembe amfungulia



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Harisson Mwakyembe leo Machi 29, 2018 ametangaza kumsamehe msanii wa muziki Roma Mkatoliki adhabu yake ya kufungiwa muziki

Msanii huyo alifungiwa kujihusisha na shughuli za muziki kwa muda wa miezi 6 kwa kosa la kutotii amri aliyokuwa amepewa na BASATA la kurekebisha baadhi ya maneno katika wimbo wa "Kibamia"

Mwakyembe amesema kuwa adhabu ya Roma itaisha muda wowote atakapokabidhiwa hati ya usajili ya Baraza la Sanaa nchini(BASATA)

Naye Roma amesema amekubali wimbo wa 'Kibamia' kutokupigwa sehemu yoyote na amevitaka vituo vya redio na runinga kufanya hivyo

0 comments:

Post a Comment