Friday 30 March 2018

Miguna amponza waziri,IGP,Mahakama yawapiga faini



Mahakama Kuu nchini Kenya imewapiga faini ya Ksh. 200,000 sawa na takribani Tsh. Millioni 4.5 kila mmoja, Waziri wa Mambo ya ndani Fred Matinag'i na Inspekta Jenerali Mkuu wa Polisi Joseph Boinnet kwa kosa la kudharau Mahakama

Jaji George Odunga aliwaamuru kufika mahakamani Jumatano, kwa ajili ya kuhukumiwa baada ya kutiwa hatiani kwa kudharau mahakama walipokataa kumuachia mwanasiasa Miguna Miguna

Faini hiyo wamepigwa bila ya wao kuwepo mahakamani na Jaji Odunga ameagiza pesa hizo zikatwe kwenye mishahara yao ya mwezi Aprili

0 comments:

Post a Comment