Tuesday 20 March 2018

Ronaldo tishio, apiga Hat-Trick



Christiano Ronaldo ameweka rekodi ya kufunga hat-trick ya 50 katika maisha yake ndani ya Real Madrid baada ya kuichapa Girona magoli 6-3 katika mechi ya ligi kuu ya Uhispania La Liga. Ronaldo alifunga bao la kwanza kwa kumalizia pasi ya Toni Kroos, Girona wakasawazisha na kufanya matokeo kuwa 1-1, Real Madrid ilifanya mashambulizi na kuongeza magoli mawili moja likifungwa na Ronaldo tena, Katika muda wa majeruhi, Christian Ronaldo aliongeza goli na kupiga hat-trick. Madrid sasa wako pointi 15 nyuma ya vinara wa ligi hiyo Barcelona.

0 comments:

Post a Comment