Tuesday 20 March 2018

Uchunguzi wa FIFA wamkata Wmbura TFF


Rais wa shirikisho la soka Tanzania (TFF) Wallace Karia amesema haya yanayotokea kwa sasa ndani ya shirikisho hilo ni miongoni mwa matokeo ya utekelezaji wa taarifa za timu ya uchunguzi kutoka shirikisho la soka duniani (FIFA). Karia ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu mwenendo mzima wa TFF, na kueleza kuwa Makamu wake wa Rais Michael Wambura amefungiwa maisha kujihusisha na masuala ya soka na kamati ya maadili ya shirikisho hilo kutokana na makosa matatu ambayo ni kupokea fedha za TFF malipo yasiyo halali, kughushi barua na kushusha hadhi ya TFF.

0 comments:

Post a Comment