Bw. Guterres amesema kila mahali wanawake wanasema wakati umefika. Wakati wa kuwepo kwa usawa, fursa na heshima, na kumaliza mabavu dhidi ya wanawake. Amesema kote duniani, wanawake na wasichana wanatoa wito wa kupambana na mateso na ubaguzi unaowakabili wakati wowote na mahali popote, na kufanya juhudi kubadilisha hali hiyo.
Ameongeza kuwa usawa wa kijinsia ni haki ya kimsingi ya binadamu na hakuna njia nzuri zaidi kujenga dunia yenye amani na utulivu zaidi, kuliko kuwawezesha wanawake na wasichana.
0 comments:
Post a Comment