Saturday 3 March 2018

TANZIA-Mtanzania auwawa nchini Afrika Kusini



Mtanzania aliyekuwa akisoma PhD katika Chuo Kikuu cha Johannesburg, Baraka Nafari ameuawa kwa kugongwa na gari kisha kuchomwa kisu
Taarifa za awali zinaeleza kuwa Watuhumiwa wa tukio hilo walishikiliwa kwa muda mfupi na kisha kuachiwa huru. Hata hivyo Jeshi la Polisi nchini humo limesema kuwa bado linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo

Akizungumzia suala hilo, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk Augustine Mahiga amesema bado ofisi yake haijapata taarifa yoyote kuhusiana na suala hilo

Raia wa Afrika Kusini wamekuwa wakiwashambulia Wageni waliopo nchini humo kwa sababu mbalimbali kwa chuki hiyo inayofahamika kama 'Xenophobia'

0 comments:

Post a Comment