Kikosi cha timu ya taifa ya
Tanzania (Tifa Stars) kimeondoka jana mchana kuelekea Algeria kwa ajili
ya mchezo wa kirafiki utakaochezwa Machi 22 mwaka huu.
Wakati kikosi hicho kikisafiri, mshambuliaji John Rafael Bocco,
ameshindwa kujumuika na wenzake kwenye safari kutokana na kuwa majeruhi
naye Hamis Abdallah amebaki kutokana na matatizo ya kiafya.
Mbali na wachezaji hao, wengine walioachwa ni Thomas Ulimwengu na Farid Mussa ambao inaelezwa wamekosa ruhusa kutoka timu wanazochezea.
Mbali na wachezaji hao, wengine walioachwa ni Thomas Ulimwengu na Farid Mussa ambao inaelezwa wamekosa ruhusa kutoka timu wanazochezea.
0 comments:
Post a Comment