Friday 30 March 2018

Urusi yalipa kisasi kwa Marekani,Yawatimua wanadiplomasia 60



Wanadiplomasia 60 wa Marekani wamefukuzwa nchini humo na Ubalozi wake uliopo St. Petersburg kufungwa kufuatia Marekani kufukuza Wanadiplomasia 60 wa Kirusi nchini kwake

Uamuzi huo wa Urusi umetanganzwa leo Machi 29, 2018 na Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov

Hii ni kufuatia muendelezo wa mvutano katika shambulio la sumu kwa jasusi wa zamani wa Kirusi pamoja na binti yake nchini Uingereza

Marekani pamoja na nchi kadhaa za Ulaya, zikiwemo Ujerumani, Ufaransa na Ukraine zilitangaza kuwafukuza Wanadiplomasia wa Kirusi katika nchi zao kwa kuishutumu Urusi kuhusika na shambulio hilo

Jasusi huyo, Sergei Skripal pamoja binti yake walikutwa wakiwa hawajitambui katika benchi jijini Salisbury, Wiltshire, Uingereza siku ya Machi 4, 2018

0 comments:

Post a Comment