Urusi inatazamia
kuwafukuza wanadiplomasia 23 wa Uingereza kutokana na mvutano
uliosababishwa na kushambuliwa kwa mpelelezi wa zamani wa Urusi na
binti yake nchini Uingereza.
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi
alisema wafanyakazi kutoka ubalozi wa Uingereza nchini Moscow wanatakiwa
kuondoshwa ndani ya wiki moja.Pia amesema ni lazima ofisi za serikali ya Uingereza nchini Urusi zinazotangaza mahusiano ya kiutamaduni kati ya nchi hizo mbili zifungwe ikiwa ni pamoja na ubalozi wa uingereza huko St.Petersburg.
Hatua ya wanadiplomasia hao kutaka kufukuzwa imekuja baada ya Uingereza kuilaumu Urusi kwa tukio lilitokea tarehe 4 mwezi machi na Urusi kukataa kuhusika kumshambulia mpelelezi wa Uingereza na binti yake.
0 comments:
Post a Comment