Rais
Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amefunguka na
kulipongeza jeshi la polisi Tanzania kwa kuweza kufanikisha kukamatwa
kwa watu ambao walikuwa wakitumia vibaya majina yake, mkewe na mtoto
wake kuwaibia watanzania.
"Natoa
pongezi nyingi kwa IGP Simon Sirro na Polisi Tanzania kwa kuwakamata
watu waliokuwa wanatumia vibaya jina langu, la mke wangu Salma na
mwanetu Ridhiwani kuwahadaa na kuwaibia Watanzania ninaowapenda sana.
Kubainika kwa mtandao huo na kukamatwa ni hatua nzuri ya kupongezwa"
alisema Jakaya Kikwete
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa
watu hao ambao wamekamatwa na jeshi hilo la polisi watafikishwa
mahakamani upelelezi ukikamilika.
0 comments:
Post a Comment