Tuesday 6 March 2018

Washiriki wa Tuzo za Oscar kutembelea Tanzania



Washiriki wa tuzo za Oscar mwaka huu kwa nyakati tofauti watatembelea Tanzania ikiwa ni moja ya zawadi kwao kwa kupendekezwa kuwania tuzo hiyo.

Mtandao wa CNBC unaripoti kuwa washiriki 25 waliopendekezwa katika vipengele vinavyopewa zawadi hiyo, kila mmoja ametengewa dola 40,000 za Marekani (takriban Sh90 milioni) kwa ajili ya safari ya kutembelea vivutio vya utalii nchini Tanzania.

Nyota hao Meryl Streep, Margot Robbie, Denzel Washington na wengine waliotajwa kuwania vipengele vya mwigizaji bora wa kike na wa kiume, mwigizaji msaidizi wa kike na wa kiume na mwongozaji bora wamezawadiwa siku 12 za kuzuru Tanzania kwa wakati watakaotaka.

Katika tuzo zinazotolewa leo Machi 4,2018 nchini Marekani, washiriki katika vipengele hivyo watapewa begi lenye zawadi ikiwamo ofa ya kuzuru Tanzania na kutembelea vivutio vya utalii watakavyochagua.

Zawadi hizo zitatolewa na kampuni ya matangazo ya Distinctive Assets ambayo ni miongoni mwa wadhamini wa tuzo hizo kwa miaka 16.

0 comments:

Post a Comment