Tuesday 17 April 2018

Mjue Alien maarufu Duniani wa kutengenezwa



Huyu ni Alien maarufu mitandaoni kama ulikua humjui anaitwa Lil Mayo, @lilmayo ni mdoli uliotengenezwa kama Alien na zishatengenezwa mamilioni ya meme kwa kutumia picha zake.

Lil Mayo yupo kwenye video mbalimbali za muziki wa rap anacheza, anavuta bangi na kunywa bia, mwaka huu ametokea kwenye nyimbo ya "Plug Walk" ya Rich The Kid, na video hiyo imetazamwa mara million 50 ndani ya mwezi mmoja.
Lil Mayo ni mtu wa kula bata sana na ameshakutana na mastaa mbalimbali duniani kama Rihanna, Tommy Chong, Chris Brown nk.


Ukurasa wake wa Instagram akitumia @lilmayo Una followers million 1 na laki 5. Alex Martyn ndio mmiliki wa alien huyu, na amechange maisha yake kupitia Lil mayo. Lil Mayo anaingiza pesa nyingi kupitia matangazo na brand yake ya nguo ya "succ".

0 comments:

Post a Comment