Tuesday 17 April 2018

Maafisa wa juu IEBC waachia ngazi



Maafisa Wakuu 3 akiwemo Naibu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi(IEBC) wamejiuzulu kwa madai ya kutokuwa na imani na Mwenyekiti wa tume hiyo, Wafula Chebukati

Wameongeza kuwa tume hiyo imeshindwa kutimiza wajibu wake na imeeingiliwa na watu kutoka nje wanaoshawishi jinsi tume hiyo inavyofanya kazi.

Maafisa hao waliotangaza kujiuzulu ni Consolata Nkatha, Paul Kurgat na Margaret Mwachanya na baada ya kujiuzulu kwao Tume ya Uchaguzi nchini Kenya sasa imebakiwa na Maafisa 3 tu

Uamuzi wa kujiuzulu kwao unajiri ikiwa ni wiki moja tu baada ya Mwenyekiti wa Tume, Wafula Chebukati kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ezra Chiloba kutokana na madai ya kuhusika na kashfa ya ununuzi wa baadhi ya vifaa vya utendaji katika tume hiyo.

0 comments:

Post a Comment