Sunday 20 May 2018

Chelsea yatwaa kombe la FA



Klabu ya Chelsea yatwaa Ubingwa wa Kombe la Chama cha Soka nchini humo(FA)

Chelsea FC imetwaa uchampioni huo baada ya kuinyuka Klabu ya Manchester United kwa bao 1 kwa nunge

Bao hilo limewekwa kimiani na mshambuliaji raia wa Ubelgiji, Eden Hazard kunako dakika ya 22 ya mchezo kwa njia ya mkwaju wa penati

Penati hiyo ilipatikana baada ya mlinzi wa Manchester United, Phil Jones, kumchezea madhambi, Eden Hazard

Mtanange huo umepigwa katika dimba la Wembley

0 comments:

Post a Comment