Saturday 5 May 2018

JPM:Kuwashughulikia wanaokula fedha miradi ya serikali



Rais Magufuli akiwa anaweka jiwe la msingi katika barabara ya Kidatu - Ifakara mkoani Morogoro amesema ni bora ule sumu kali lakini si kula hela ya Serikali ya awamu ya tano.

Amesema kuna maeneo ambapo wakandarasi wamekula hela za miradi na anawaona kama wamekula sumu kwani hatojali fisadi ametoka CCM, CHADEMA wala CUF au nje ya nchi atawashughulikia.

"Hela ya Serikali ya awamu ya tano hailiwi bora ule sumu kali. Waliokula fedha waaanze kujiandaa, kurudisha fedha na kutekeleza miradi au kukumbana na sheria ya mwaka 97." alisisitiza Rais Magufuli.

"Haiwezekani mimi nitafute hela halafu wewe uzile tu nikwambie umeula wa chuya. Kama makandarasi watakuwa wamekimbia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, Polisi na TAKUKURU wawatafute popote. Watazitapika hizo fedha wanazozitafuna"

0 comments:

Post a Comment