Friday 1 June 2018

Zidane aukacha Ukocha rasmi



Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane maarufu Zizou ametangaza kujiuzulu kuendelea kuifundisha miamba hiyo ya soka Duniani leo Mei 31, 2018

Zidane ametangaza hivyo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari aliouitisha ghafla ikiwa ni siku tano tangu kushinda Kombe lake 3 la UEFA Champions League ikiwa kama kocha wa klabu hiyo

Zidane ambaye amekaa na klabu ya Real Madrid kwa zaidi ya miaka miwili tangu alipotangazwa kocha wa timu hiyo Januari 4, 2016 ameipatia jumla ya makombe 9

Makombe hayo ni UEFA Champions Leagues(3), Club World Cups(2), European Super Cups(2), League(1) na Spanish Super Cup(1)

Zizou akiwa Kocha wa Madrid ameiongoza timu hiyo katika michezo 149, ameshinda michezo 104, ametoa droo michezo 29 na kufungwa michezo 16. Asilimia zake za ushindi ni 69.79%

0 comments:

Post a Comment