Thursday, 3 May 2018

Wajawazito wakatazwa kuvaa shela siku ya ndoa



Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha, limepiga marufuku wajawazito kuvaa shela wakati wa kufunga ndoa kwa kuwa vazi hilo ni alama ya ubikira kwa mwanamke

Paroko Msaidizi wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Theresa, Padri Festus Mangwangi, alisema hayo jana akiweka mkazo juu ya tamko lililotolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo hilo, Isaack Amani, wakati akiadhimisha misa ya shukrani iliyofanyika Jumapili iliyopita

Askofu Amani alisema wazazi wanatakiwa kuwafundisha watoto wao wa kike kutunza miili yao na kuishi maisha ya kimaadili hadi watakapopata wenza wa kufunga nao ndoa na hapo ndipo alama ya shela itakapoonekana umuhimu wake

Padri Mangwangi alisema atakayedanganya na kuvaa shela wakati tayari anamjua mwanamume au ni mjamzito atakuwa anafanya utovu wa nidhamu

0 comments:

Post a Comment