Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekanusha taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa wanafunzi ambao wazazi wao wana leseni za biashara hawataruhusiwa kupata mkopo wa elimu ya juu
Wakati akiongea na Waandishi wa habari leo Mei 11, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole-Nasha amesema kuwa taarifa hizo sio za kweli na kuutaka umma kuzipuuza
Naibu Waziri, Ole-Nasha ameendelea kwa kusema "Vigezo vinavyotumika kutoa mkopo vinabadilika kila mwaka kulingana na maboresho yanayofanywa ili kuendana na wakati"
Mwaka huu matarajio ni kutoa mkopo kwa wanafunzi 122,000 na kati yao 30,000 ni wa mwaka wa kwanza na 80,000 ni wanafunzi wanaoendelea na masomo yao
0 comments:
Post a Comment