Friday 8 June 2018

Baba yake Drake amjia juu Pusha T



Baba yake Drake amjia juu Pusha T, adai hamfahamu mtu yoyote anayeitwa Pusha “If i knew i would push their T”

Wakati Drake akiwa kimya na kuipotezea diss ya Pusha T “The story of Adidon” Baba yake amemsaidia kazi

TMZ walikutana na mzee, Dennis Graham na wakamtaka aongelee bifu kati ya mwanae na Pusha T

Baba yake Drake aliwajibu kuwa hamfahamu Pusha T, alisema hajui chochote kuhusu mtu anayeitwa Pusha T “ I dont know anybody named Push-T, If i did, I would Push their T”

Hatahivyo alikuwa mhanga wa Diss ya Pusha T, alidai kuwa Drake amemtelekeza mtoto wake kwasababu hata yeye baba yake alimtelekeza akiwa na miaka 5 “Your father walked away at 5, hell of a dad thing”

0 comments:

Post a Comment