Thursday 28 June 2018

Baba yake Michael Jackson, Joe Jackson afariki Dunia



Joe Jackson, Baba Mzazi na aliyekuwa Meneja wa Michael Jackson amefariki dunia.

Ikiwa imepita siku 1 tangu dunia iazimishe miaka 9 ya kumpoteza mfalme wa Pop, Michael Jackson, Leo Baba yake mzazi Joe Jackson amefariki akiwa na umri wa miaka 89.

TMZ wameripoti kuwa #JoeJackson alikuwa akipambana na ugonjwa wa Cancer, wameripoti kuwa tangu mapema mwezi huu Joe alikuwa amelazwa hospitali.

Joe alikua akipambana na matatizo ya afya kwa muda, Hali yake ya kiafya ilianza kuwa mbaya Mwaka 2015 baada ya kushambuliwa na kiharusi na kupata mashambulizi ya moyo (Heart attack) mara 3, mwaka 2016 pia alilazwa lakini alipata nafuu.

0 comments:

Post a Comment