Wakongwe wawili kwenye mchezo
kwa upande wa wanawake duniani, Serena Williams wa Marekani na Maria
Sharapova wanakutana leo katika mechi ya raundi ya nne katika michuano
ya Ufaransa inayoendelea mjini Paris.
Wawili hao walifuzu baada ya kushinda mechi zao za raundi ya tatu Serena akimshinda Julie Gorges wa Ujerumani na Maria dhidi ya Karolina Pliskova wa jamhuri ya Czech.
Tangu wawili hao waanze kukutana uwanjani, wamecheza mechi 21, Serena akishinda 19 na Maria akishinda 2 pekee.
Mechi hii inatazamiwa kuwa yenye ushindani mkubwa kwa kuwa wote wamewahi kuwa namba moja kwa viwango vya ubora duniani, na kila mmoja kwa sasa maerejea baada ya kutocheza kwa muda mrefu.

0 comments:
Post a Comment