Thursday 28 June 2018

Taarifa za Oprah kwenda Kenya zagonga mwamba



Taarifa ya furaha iliwafikia Wakenya kuwa Mwanamama tajiri duniani, Oprah Winfrey ataikanyaga ardhi yao kwa mara ya kwanza.

#Oprah alitajwa kuwepo kwenye msafara wa ugeni wa Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama ambaye ametajwa kuwasili nchini Kenya Julai 16 mwaka huu kwa shughuli mbili: Kuitembelea ikulu ya Kenya ambapo atatunukiwa tuzo ya heshima pia baadae atakuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya Uzinduzi wa NGO ya dada yake, Dr. Auma Obama itakayo fanyika kijijini kwao, K'Ogelo.

Sasa taarifa rasmi kutoka kituo cha Televisheni cha CNN zimeripoti kuwa, Oprah Winfrey hatokuwepo na taarifa zile za awali zilikuwa ni uzushi mtupu
"But it's not accurate that Oprah will go (Just to be clear on that, since it's been a widely circulated rumor) " ilisomeka email ya msemaji wa Obama.

Lakini kifuta machozi ni kuwa, ugeni huo unatarajiwa kuchagizwa na uwepo wa Muimbaji mwenye asili ya Senegal, AKON pamoja na mkongwe wa muziki kutoka nchini Zimbabwe, Oliver Mutukudzi.

0 comments:

Post a Comment