Sunday 19 August 2018

Dele Ali aiteka Dunia



Challenge ya mchezaji wa Tottenham Hotspurs Dele Ali @dele yafunika challenge zote zinazotrend kupitia mitandaoni.

Kwa Muonekano ni rahisi lakini sio kama inavyozaniwa ni kati ya challenge ngumu kuwahi kutokea, inakuitaji kukunja vidole vyako viwili kidole gumba na kidole cha kwanza huku vidole vitatu vikiwa juu ya paji lako uso na vikiwa vimenyooka.

Mastaa mbalimbali wameonyesha umahiri wao lakini Mchezaji Musa Dembele aliona isiwe shida na kuweka kikaratasi kuonesha kuwa ameweza.

Dele Ali aliianza challenge hiyo baada ya kuipatia ushindi timu yake dhidi ya Newcastle hivi karibuni na kufanya kuwa moja kati ya ushangiliaji uliokuwa gumzo mitandaoni.

Gazeti mashuhuri kutoka nchini Uingereza la The Standard limeandika kuwa challenge ya Dele Ali imeishusha challenge ya Shaggy kupitia nyimbo ya Drake #inmyfeelingschallenge.

Hapa nchini Tanzania msanii @diamondplatnumz ameanzisha challenge ya kudansi kupitia ngoma yao mpya ya #Jibebe huku akiahaidi kutoa million 2 kwa mshindi.

0 comments:

Post a Comment