Saturday 18 August 2018

Koffi Anan Afariki Dunia

  •  
    Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN), Kofi Annan amefariki dunia akiwa na miaka 80
    -
    Mwanadiplomasia huyo amefariki asubuhi ya leo nchini Uswisi baada ya kuugua kwa muda mfupi
    -
    Kutokana na umahiri wake Kofi Annan alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Desemba 1996. Na alianza kazi rasmi Januari 1, 1997
    -
    Mwaka 2001 alichaguliwa kwa mara ya pili kuuongoza tena Umoja wa Mataifa. Oktoba 12, 2001 alitunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel
    -
    Annan alianza kutumikia nafasi mbalimbali ndani ya Umoja wa Mataifa(UN) tangu mwaka 1974 ingawa aliacha kazi na kurudi kuiongoza Kampuni ya Utalii nchini mwake
    -
    Mwaka 1976 alirudi tena kwenye ulingo wa siasa za kimataifa na safari yake ndani ya Umoja wa Mataifa ikaanza rasmi
    -
    Kofi Atta Annan alizaliwa Aprili 8, 1938 nchini Ghana

0 comments:

Post a Comment