Sunday 26 August 2018

Rais mstaafu Jakaya Kikwete kumuwakilisha JPM Zimbabwe



Rais Magufuli amemtuma Rais mstaafu wa awamu ya 4, Jakaya Kikwete kumuwakilisha kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa

Ataambatana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Philip Mangula na Mwenyekiti chama cha UDP, John Cheyo

Emmerson Mnangagwa alitangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi uliofanyika Julai 30 mwaka huu

Mnangagwa alimshinda mgombea wa upinzani kupitia chama cha Movement for Democratic Change(MDC), ndugu Nelson Chamisa

Katika uchaguzi huo Mnangagwa kupitia chama kikongwe cha ZANU-PF alipata asilimia 50.8 ya kura zote huku Nelson Chamisa akipata asilimia 44.3 ya kura zote

0 comments:

Post a Comment