Thursday 30 August 2018

Spika Kadaga wa Uganda Acharuka



Spika wa Bunge nchini Uganda Rebecca Kadaga amemtaka Rais Yoweri Museveni kuwashtaki maofisa usalama waliowatesa Wabunge na Wanahabari wakati wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi mdogo wa Arua.

Hatahivyo Spika Kadaga amesema kuwa iwapo Rais huyo asipofanya hivyo anawaweka wabunge wake katika wakati mgumu wa kufanya shughuli zao za kutumikia taifa.

Siku chache zilizopita mbunge na msanii Mh Bobi Wine inadaiwa alipigwa na maafisa wa usalama kipindi alichokuwa mahabusu.
.

0 comments:

Post a Comment