Thursday 30 August 2018

Waziri Mwijage azindua Bodi Mpya ya TPSF


NA ISDORY NJAVIKE
WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage ameitaka
Bodi mpya ya Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) kushikana na
serikali kuijenga Tanzania itakayokuwa na uchumi wa kati, shirikishi
na viwanda ifikapo mwaka 2025.

Akizundua Bodi mpya  ya TPSF jijini Dar es Salaam, Waziri Mwijage
ameiambia bodi mpya kuwa imepewa jukumu kubwa na sekta binafsi
iliwafanye kazi kwa bidii na kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi hapa
Tanzania ikiwemo kuoengoza mapato ya serikali, ajira na kuweka misingi
mizuri kwa ustawi wa sekta hiyo.
"Tumefanya mabadiliko katika bodi hii ya TPSF na mnatakiwa kujuwa jukumu kubwa ambalo mmepewa ni jukumu la kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi katika kuhakikisha  maongeza mapato nchini yatakayo tokanna na kazi mnazofanya," alisema Waziri Mwijage
Uzinduzi huo wa Bodi mpya ulitanguliwa na uchaguzi ambao Bw. Salum
Shamte alichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya TPSF na Bi. Angelina Ngalula
kuwa Makamu Mwenyekiti. Bw.Shamte amechukua nafasi ya Dkt. Reginald
Mengi ambaye muda wake umemalizika.

Kwa upande wake Mwenyekiti mpya, Bw. Shamte mbali ya kuwashukuru
wajumbe wote kwa kumchangua kuwa mwenyekiti, amesema sekta binafsi
lazima itoe mchango mkubwa katika kujenga Tanzania mpya kiuchumi.

Wajumbe waliochanguliwa kwenye bodi hiyo ni Bw. Subhash Patel, Dkt.
Charles Kimei, Fatma Kange, Bw. Dhrur Ashtosh Jog, Bw. Sylivestry
Koka, Bw. Peter Shayo, Bw. Octavian Mshiu,Bw.Abdulsamad Abdulrahim,
Bi. Jacquiline Mkindi na Bw. Sanjay Rughani.
Mwisho.

0 comments:

Post a Comment