Thursday 9 August 2018

TANZIA: Msanii Mkongwe wa vichekesho, Amri Athuman maarufu King Majuto amefariki dunia



 Msanii Mkongwe wa vichekesho, Amri Athuman maarufu King Majuto amefariki dunia usiku wa leo Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili alipokuwa anapatiwa matibabu
-
Jumanne ya Julai 31, Mzee Majuto alipelekwa hospitalini hapo na kulazwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum(ICU)
-
Hiyo ilikuwa mara ya pili kwa Mzee Majuto kulazwa hospitalini hapo, mara ya kwanza alilazwa kabla ya kwenda India kwa ajili ya matibabu
-
Muigizaji huyo alizaliwa mwaka 1948 jijini Tanga na kusoma shule Msambwini mkoani humo, alianza kuigiza 1958 akiwa na umri wa miaka 10

0 comments:

Post a Comment