-
Sonia Fanuel mkazi wa Nyegezi jijini Mwanza anashikuliwa na Polisi kwa kukutwa na funguo bandia 53 za vitasa pamoja na 101 za Makufuli
-
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Jonathan Shanna amesema msichana huyo alikamatwa Septemba 13 saa 1:45 jioni mtaa wa Rose Kata ya Nyegezi
-
Shanna alieleza kuwa Sonia alikamatwa baada ya wasichana wawili, Esther Isaack na Ruth Sumari kukuta milango ya vyumba vyao imefunguliwa huku mtuhumiwa akiwa amejibanza ukutani
-
Amesema Wasichana hao walipokagua mali zao ndani walibaini Tsh. 160,000 zimeibwa na nguo zenye thamani ya Tsh. 200,000
0 comments:
Post a Comment