Sunday 29 October 2017

Anthony Joshua azua kizaazaa baada ya kumdunda Mfaransa




Mwanandondi kutoka nchini Uingereza Anthony Joshua amemshinda Carlos Takam raia a Ufaransa katika pambano la uzito wa juu kuwania mkanda wa IBF lililomalizika leo kwenye Uwanja wa Cardiff.




Tekam alionekana kushindwa kuvumilia makonde makali kutoka kwa Joshua katika raundi ya 10 na ikapelekea kushindwa kuendelea na pambano hilo na mwisho mwendeshaji alimtangaza Joshua kama mshindi.

  Hapo awali Joshua alipangwa apigane na Kubrat Pulev lakini aliumia na kujitoa na Takam akachukua nafasi yake.



Ingawa alibezwa na wengi, Mfaransa huyo alionyesha kiwango kizuri na usugu licha ya kwamba Joshua alipiga ngumi nyingi zaidi.

Mabondia hao waligongana vichwa mapema kabisa, lakini walijitahidi kuendelea kupambana hadi raundi ya 10 Takam aliposhindwa.

0 comments:

Post a Comment