Monday 30 October 2017

Irene Uwoya amthibitisha mume wake kuwa ni Dogo Janja

Baaada ya mashabiki kuwa na maswali mengi leo kupitia mtandao wa Instagram msanii wa Bongo Movie Irene Uwoya amethibitisha tetesi za kuwa amefunga ndoa na Dogo Janja.
Ameandika kwenye Instagram kuwa ana furaha kubwa kuolewa na msanii mwenye miondoko ya kuchana (Rap) na  ambaye ni mwanaume wa ndoto yake.

Uwoya-2 

Kabla ya hapo, Irene Uwoya alikuwa ameolewa na mchezaji anayeichezea timu ya Taifa ya Burundi (Ntamba murugamba ) Hamad Ndikumana na kujaaliwa kupata mtoto mmoja.

0 comments:

Post a Comment