Monday 27 November 2017

Lady Jaydee ajiunga rasmi na lebo mpya kutoka Kenya


Mwanamuziki mkongwe kutoka nchini Tanzania jidejaydee leo amethibitisha kusaini mkataba na Taurus Music moja kati ya Lebo kubwa kutoka nchini kenya.
Amethibitisha hayo kupitia instagrama yake.
"Mara ya kwanza kabisa ku sign na record label ilikuwa 2001 ambapo nili sign mkataba wa Albums 2.
Album yangu ya kwanza Machozi na album ya pili Binti  Baada ya hapo sikuwahi ku sign tena mkataba mwingine wowote hapo katikati, Bali nilikuwa nafanya kazi na ndugu jamaa na marafiki wa karibu ambao nawashukuru sana kwa mchango wao mkubwa katika kuniendeleza na kunipa moyo.
✌✌✌✌
Ninapoufunga mwaka 2017 naufunga kwa Neema ya kipekee kwani kwa mara ya pili katika career yangu ya muziki nime sign na @taurusmusik na natarajia mambo makubwa zaidi ya hapo nyuma kwani kila hatua naamini inatakiwa kukusogeza katika kupanda juu zaidi
Mapenzi tele kwa fans, family, kila mmoja ambae amechangia mimi kuwepo hapa bila kutaja jina la mmoja mmoja , na hata wale tuliotofautiana lakini bado walichangia kufanikiwa kwangu hata kama ni 1% ( huo ni ubinaadam )na watu wote wenye imani na Lady JayDee ✌❤️
Ila Mama yangu mzazi ndio mwanamke pekee anaenipa nguvu na sababu ya kuendelea mbele kila kukicha ❤️Nani Kama Mama ?❤️ #TunasongaMbeleHaturudiNyuma
#SikuYaKuchokaNdioSikuYaKufa
#KeepTheFireBurning 
Prepared by @msa_ulimoney_______ #newschemba #legendjide

0 comments:

Post a Comment