Tuesday 7 November 2017

Nyalandu amtembelea Lowassa aahidi kuendelea kufata nyayo zake

Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Lazaro Nyalandu amemtembelea Waziri Mkuu wa zamani na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa ofisini kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Nyalandu aliyejiondoa CCM wiki iliyopita leo amemshukuru Lowassa kwa kuonyesha njia kwa wengine kuwa kuna maisha nje ya CCM.

“Mzee wangu nimekuja kujitambulisha na kusema asante kutufungulia mlango,” amesema Nyalandu katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya Lowassa.

Kwa upande wake, Lowassa aliyetoka CCM mwaka 2015 amemkaribisha Nyalandu upinzani akisema, “Nimefarijika kuja huku karibu sana tushirikiane na kwa hakika 2020 tutavuka daraja.”

0 comments:

Post a Comment