Wednesday 29 November 2017

Prince Harry,Meghan ndoa mwezi Mei mwakani

Mwanamfalme Harry na Meghan Markle wanatarajia kufunga ndoa katika kanisa ndogo la St George, Windsor Castle mwezi Mei mwaka ujao, Kensington Palace imetangaza.

Familia ya kifalme nchini Uingereza itagharimia harusi hiyo, ikiwa ni pamoja na ibada yenyewe, muziki, maua na sherehe ya baada ya ibada.

Bi Markle, ambaye ni mprotestanti, atabatizwa na kupewa kipaimara kabla ya harusi hiyo kufanyika, kasri hilo limetangaza.
Mwigizaji huyo Mmarekani pia anakusudia kuchukua uraia wa Uingereza.
Afisa wa mawasiliano wa Mwanamfalme Harry Jason Knauf amesema Windsor ni "pahala maalum sana" kwa wawili hao, akisema walikaa huko kwa muda tangu walipokutana mara ya kwanza Julai 2016.
Amesema Prince Harry na Bi Markle watatekeleza majukumu yao ya kwanza rasmi kwa pamoja Nottingham Ijumaa.

0 comments:

Post a Comment