Tuesday 14 November 2017

Ukweli wangu unanigomanisha na watu- Baraka The Prince



Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Barakah The Prince amesema hajawahi kugombana na msanii yeyote ila kusema kwake ukweli ndio kunafanya watu kumchukulia kama mkorofi.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Sometimes’ amekiambia kipindi cha XXL, Clouds Fm kuwa baada ya kuligundua hilo ameamua kulifanyia kazi.
“Sijawahi kugombana na wala kumtukana na msanii mwenzangu  but nahisi ukweli wangu kwa watu ndio tatizo , unajua watu wengi hawapendi kuambiwa ukweli, anaweza akakuboa ukamwambia ukweli akakuchukulia tofauti kwa hiyo nadhani sana hiyo ndio ilikuwa inachangia” amesema Barakah.
“Wakati huu nimejitahidi ndio maana hata nimekaa kimya muda mrefu sana, nimejaribu kukaa na watu wengi sana wamenipa ushauri wakiwemo watu wakubwa kwenye entertainment” aliongeza Barakah.

0 comments:

Post a Comment