Tuesday 12 December 2017

Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars awaomba radhi mashabiki


Hayo yametokea baada ya Tanzania bara 'Kilimanjaro Stars' kutolewa kwenye mashindano ya Cecafa nchini Kenya, kocha wa timu hiyo Ammy Ninje amewaomba radhi watanzania kwa matokeo mabaya iliyopata timu yao kwenye michuano hayo.
Kili Stars imetolewa ikiwa inaburuza mkia katika Kundi A lililokuwa na timu tano, timu hiyo imeambulia pointi moja iliyoipata baada ya kutoka suluhu dhidi ya Libya kwenye mchezo wa kwanza. Matumaini yalianza kupotea kufuatia kuchapwa 2-1 na Zanziba kabla ya vipigo vingine kutoka kwa Rwanda (2-1) na Kenya (1-0).
Licha ya matokeo mabaya katika michuano ya Cecafa, Ninje amabye ni kocha wa zamani wa shule ya michezo ya Hull City nchini Uingereza amesema hana mpango wa kung'atuka kwa kuwa anaamini timu hiyo itarejea makali yake.

0 comments:

Post a Comment