Mahakama
ya juu zaidi nchini Hispania imefuta hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa
aliyekuwa kiongozi wa Catalonia, Carles Puigdemont aliyeondolewa
mamlakani pamoja na wajumbe wengine wanne wa iliyokuwa serikali ya eneo
hilo.
Mahakama hiyo ilitangaza uamuzi huo jana Jumanne. Awali, mahakama hiyo ilikuwa imeziomba mamlaka za Ubeligiji kuwarejesha nyumbani watu hao watano walioikimbia Hispania baada ya kuondolewa mamlakani kufuatia kujitangazia uhuru wa upande mmoja. Tuhuma wanazokabiliwa nazo ni pamoja na uasi na uchochezi.
0 comments:
Post a Comment