Wednesday 6 December 2017

Rais Trump kutangaza Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel


Rais Trump kutangaza Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel

Maafisa waandamizi wa serikali ya Marekani wanasema Rais Donald Trump wa nchi hiyo ameamua kulitambua jiji la Jerusalem kama mji mkuu wa Israel na kwamba siku zijazo atahamisha ubalozi wa nchi yake kutoka jiji la Tel Aviv ulipo sasa na kuupeleka jijini Jerusalem. Trump anatarajiwa kutangaza rasmi uamuzi huo leo Jumatano.

Israel imekuwa ikidai jiji la Jerusalem kuwa ni mji wake mkuu lakini jumuia ya kimataifa haitambui jiji hilo kama mji mkuu wa nchi hiyo.

Uamuzi wa Rais Trump ni dhahiri utawakasirisha Wapalestina na mataifa ya Kiarabu na utakuwa na athari kubwa kimataifa.

 Hatahivyo uamuzi huo umeonekana kupigwa vikali na mataaifa jirani ya Israel wakidai kuwa watakosa huduma alizokuwa wanazipata kutoka mji huo.

0 comments:

Post a Comment